info@parokiaboko.or.tz

(+255) 754 348 651

Historia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja

Mwenye Heri Isidori Bakanja

Maisha ya Utoto
Isidore Bakanja alizaliwa mwaka 1887 katika kijiji cha Bokendela, miongoni mwa kabila la Boangi, huko Kongo. Alibatizwa tarehe 6 Mei 1906, akiwa na umri wa miaka 18.

Upendo kwa Bikira Maria
Mwenye Heri Bakanja alimpenda sana Mama Maria. Alisali Rozari kila alipopata nafasi na alipenda kuvaa skapulari ya Bikira Maria wa Karmeli kila wakati.

Changamoto katika Kazi
Alifanya kazi katika shamba la mzungu (Mbelgiji). Msimamizi wa shamba hilo alimkataza kuhubiri Injili kwa wafanyakazi wenzake na pia alimzuia kuvaa skapulari yake.

Mateso kwa Imani
Mwenye Heri Isidore alikataa maagizo ya mwajiri wake na aliendelea kuvaa skapulari na kuhubiri Injili. Kwa sababu hiyo, mwajiri wake aliagiza akamatwe na apigwe vikali.
Baada ya kipigo kikali, alipelekwa hospitalini kwa matibabu, lakini madaktari walithibitisha kuwa walishindwa kumtibu kwa sababu ya maambukizi makubwa aliyopata.

Kifo cha Ushuhuda
Alipozidiwa sana, alisema:
👉 “Ninakufa kwa sababu ya Ukristo wangu.”

Wamisionari walipomtembelea, walimsihi awasamehe waliomtesa. Alijibu kuwa tayari ameshawasamehe, na akisema kuwa akifika Mbinguni atawaombea.

Utakaso
Mwenye Heri Isidore Bakanja alifariki dunia tarehe 15 Agosti 1909.
Tarehe 24 Aprili 1994, alitangazwa kuwa Mwenyeheri na Papa Yohane Paulo II.


Na mwanga wa Mungu umuangazie daima!